TLS Wamvimbia Mwanasheria mkuu wa Serikali, yasema uchaguzibutafanyika kwa kanuni za zamani
Chama cha Wanasheria cha Tanganyika Law Society (TLS) kimesema uchaguzi wa viongozi wa TLS utafanyika kwa muongozo wa kanuni za zamani na si mpya ambazo zimetolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Kauli hii imetolewa katika kipindi ambacho wanachama kadhaa wa chama hicho wamejitokeza kutangaza nia ya kuwania nafasi ya Uraisi wa TLS, Fatma Karume na Godwin Ngwilimi ni moja kati ya wanachama wa TLS ambao wameonesha nia ya kurithi kiti hicho cha uraisi ambacho sasa kipo chini ya Tundu Antipas Lissu. Bwana Ngwilimi amesema wao kama viongozi wa TLS wako tayari kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya kanuni hizo kama serikali itashinikiza kanuni mpya zitumike ndani ya TLS.Nae Fatma Karume yeye amejikita zaid kwenye utetezi wa haki za binadamu hasa Police brutality, ameelezea mfano wa Polisi kumshikilia mtuhumiwa kituoni kwa siku 14 bila kumpeleka mahakamani, anasema TLS ndo chombo pekee cha kuhakikisha nchini kunakuwa na "Rule of Law" hivyo akiwa Rais atapambana na mambo hayo. ...