Hotuba ya Raisi Magufuli wakati wa uzinduzi wa ukuta kwenye Migodi ya Tanzanite huko Mererani Mkoani Manyara.


Update;
Msafara wa Rais Magufuli sasa unaelekea Mirerani, karibia Runinga yako ushuhudie matukio live kupitia TBC sasa!
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti anaingia kutoa salamu na kuwatambulisha viongozi mbalimbali wa Serikali na wa Kijeshi na wadau wengine waliohudhuria uzinduzi huo
Mkuu wa mkoa anamshukuru Rais Magufuli kwa ujenzi wa ukuta huo ambao utazuia utoroshwaji wa madini na kuokoa mapato mengi
Anasema pia wachimbaji wadogo awali walikuwa hawalipi kodi kabla ya ujenzi wa ukuta huo ila sasa wameshaanza kulipa
Pia gari la kubebea wagonjwa katika mji mdogo wa Mrererani limenunuliwa na pia wizara ya maji imeanza kuchimba visima kwa ajili ya kutatua tatizo la upatikanaji wa maji.
Mkuu wa jeshi la kujenga taifa (JKT) Martini Busungu anatoa taarifa ya ujenzi wa ukuta huo, anaanza kwa kutambua uwepo wa viongozi wa kiserikali na kijeshi waliohudhuria uzinduzi huo
Anamshukuru Mkuu wa majeshi ya Ulinzi, Evance Mabeyo kwa kuanza kutoa maagizo juu ya ujenzi wa ukjuta huo baada ya rais kusema ujengwe
Anashukurukuru pia kwa Tanroads, taaisis ya wahandisi Tanzania, kiwanda cha Saruji Tanga kwa kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya mradi huo
Anasema ujenzi wa ukuta huo umejengwa kwa utaalamu wa kutosha kwa kutumia wataalamu wake wa jeshi
Gharama za ujenzi wa maradi huo ni Shilingi 5,645,843,163, mradi huo ulikabiliwa na changamoto kama ujenzi kwenye miamba na makorongo na uwepo wa mito ya misimu
Ujenzi huo ulifanyika kwa njia ya operesheni ambapo vijana wa JKT walitumika katika ujenzi na kutoa maelekezo ya kitaalamu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mabeyo
Anasema leo taifa hili limeweka historia itakayodumu milele, ukuta huo uliagizwa kujengwa mwezi Septemba mwaka 2017 na ujenzi kuanza mwezi Novemba.
Maagizo hayo yametekelezwa na kazi imekamilika na watamkabidhi Rais ndani ya muda mfupi ujao, ukuta huo una urefu wa kilomita 24.5 na ulianza kujengwa mwezi Novemba mwaka 2017 na kukamilika mwezi Februari mwaka 2018
Waliokamilisha ujenzi huo ni waandisi kutoka JKT pamoja na askari wa JKT
Fedha zilizotumika kujenga zinaoweza kuonekana ni nyingi, ila gharama hizo zitaonekana ni ndogo ukuta huo utakapoanza kuleta manufaa
Taifa linapaswa kujivunia kutokana na ujenzi wa ukuta huo, matokeo ya ujenzi wa ukuta huo yanaonyesha kuwa jukumu la jeshi sio kulinda mipaka ya nchi na katiba ya nchi tu, bali pia kushiriki katika ujenzi wa miradi inayosaidia taifa
Katika utekelezaji wa jukumu hilo kumejidhihirisha, uzalendo, umoja na mshikamano katika watanzania wapenda maendeleo, kwani walipata msaada kutoka katika wananchi wa eneo la Mererani
Pia JKT wametumia uwezo wao kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi wa hali ya juu
Jeshi limeonyesha nidhamu ya juu katika uchapaji kazi katika utekelezaji wa maagizo yanayotolewa, mradi huo ulipangwa kukamilika ndani ya miezi 6 ila ulkikamilika katika miezi 3
Maagizo pia ya ujenzi wa ukuta katika uwanja vita wa Ngerengere nao unajengwa na upo katika hatua za mwisho, ukuta huo una urefu wa kilometa 14 na wanaoshiriki katika ujenzi huo ni vijana waiojenga ukuta wa Mererani
Mkuu wa majeshi anahitimisha kwa kusema muda wowote wapo tayari kutekeleza maagizo yoyote yatakayoagizwa kwa ajili ya maslahi ya nchi
Waziri wa Ulinzi, Hussein Mwinyi anaongea
Anamshukuru rais kwa imani aliyonayo kwa jeshi Tanzania na wizara yake, na pia kukubali kuhudhuria uzinduzi wa ukuta huo licha ya kua na majukumu mengi
Anasema ukuta huo utakuwa historia katika nchi yetu kwani eneo lenye rasilimali muhimu ya nchi linalindwa kwa kujengewa ukuta
Anashukuru jeshi la Tanzania kwa utekelezaji wa ujenzi huo kwa weledi na ndani ya muda mfupi
Pia anashukuru wananchi kwa kutoa ushirikiano kwa jeshi wakati wa ujenzi wa ukuta huo hadi ukakamilika
Anamkabidhi Rais hati na ufunguo kama ishara ya kukamilika kwa ukuta huo
Waziri wa madini, Angela Kairuki nae anaingia kuongea
Anamshukuru rais kwa kukubali mualiko na kuja kuzindua ukuta huo
Anasema wananchi waliokusanyika wana shauku kubwa ya kumuona na pia anashukuru jeshi kwa kazi na utii walioonyesha
Anampongeza rais kwa uongozi thabiti amabao umeweza kufanyika kwa mapinduzi katika sekta ya madini na kuhakikisha rasilimali za madini zinalindwa ipasavyo
Amesema pia madini yalikuwa yakitoroshwa na kuongozewa thamani na kuzinufaisha nchi hizo na sasa Tanzania inaona mwanga kutokana na juhudi za Rais
Anashukuru bunge kwa kuunda kamati na kutoa mapendekezo yaliyopelekea kutungwa kwa sheria inayotaka madini yasitolewe nje ya nchi kabla ya kuongezewa thamani
Wizara ya madini sasa inaandaa kanuni za Mererani Contolled Area ambazo zitakua zinatoa muongozo wa namna madini yatakavyochimbwa na kulindwa hadi yatakapuzwa katika mgodi wa Mererani
Pia kwa sasa wameandaa vitambulisho ambavyo vitatolewa kwa wachimbaji wa madini, jumla ya watu 6500 wameweza kusajiliwa na zoezi linaendelea
na kuishukuru NIDA kwa kuwezeshautoaji wa vitambulisho hivyo kwa wakati
Kipindi cha nyuma mrabaha kutoka uchimbaji wa madini ukiacha Stamico na Tanzanite One ilikuwa ni milioni 166.8 mwaka 2015 na mwaka 2016 ilikuwa ni milioni 71.8 lakini kwa miezi mitatu pekee tangu maelekezo yatolewe mrabaha umekuwa ni milioni 714 ambapo ni takribani mara nne ndani ya miezi mitatu tu
Ndani ya ukuta huo kutakua na eneo la uchimbaji, eneo la uonezeaji thamani madini, eneo la burudani na shughuli nyingine
Pia kutakua na kujenga miundombinu ya ulinzi kuzunguka ukuta kama umeme na kamera
Rais Magufuli anaingia kuongea
Anawasalimia viongozi mbalimbali wa serikali, wa kijeshi, wadau na wananchi waliohudhuria
Anawashukuru viongozi wa jeshi kwa kumkaribisha kuzindua na kukamilisha ujenzi wa ukuta huo chini ya wakati uliopangwa
Anampongeza Jenerali Mabeyo kuwa hicho ndio kilikuwa kipimo chake na amekishinda, maana hakuna aliyetegema ukuta huo kuchukua muda mfupi hivyo
Anasema wangeweka kandarasi ukuta huo ungechukua zaidi ya mwaka na vifaa vya ujenzi vingeibiwa
Rais anasema maombi yaliyoombwa hapo kuhuhusu kuwafukiria vijana waliojenga ukuta huo ni ngumu kuyakataa
Anashukuru wizara ya madini na ulinzi na majemedari wote hadi wa ngazi ya chini kwa jinsi walivyosimamia ujenzi wa ukuta huo
Anaahidi kwa Waziri wa Ujenzi na CDF kuwa atatoa barua yake yakuwashukuru walioshiriki ujenzi wa ukuta huo na ataangalia utaratibu mzuri wa kuwapongeza
Amesema vijana wa JKT walioshiriki kujenga ukuta huo watachukuliwa kwenye majeshi ya ulinzi na polisi kama shukrani kwa ujenzi wa ukuta huo
Rais anasema alikuwa anasikia wananchi wa imanjiro walikuwa hawana gari la wagonjwa na amekuja nalo na atamkabidhi mkurugenzi
Rais anasema ameambiwa tangia madini hayo yagunduliwe na mzee Jumanne Ngoma mwaka 1967, na barua ya Nyerere na barua ya Mjiolojia zilizondikwa kuonyesha kutambua ugunduzi huo ameziona ila bado ana maisha magumu[ Jumanne Ngoma: Mgunduzi wa Tanzanite anayetaabika, rais Magufuli amshika mkono]
Hii inaonyesha Tanzanite haikugunduliwa na mtu kutoka nje, ila mtanzania huyo anaishi maisha magumu na ameparalaizi
Rais anasema naye amaegundua aiana fulani ya kemikali pia ila hajatambuliwa
Anataka mzee huyo apande jukwaani kama anaweza kuja ili atambuliwe kuwa yeye ndio mgunduzi wa madini ya Tanzanite (anapelekwa kwenye meza kuu)
Rais Magufuli anasema serikali itampa mzee huyo Shilingi milioni 100 ili akazitumie katika matibabu yake na shughuli nyingine
Rais anatoa wito kwa Watanzania kuwathamini wanaofanya mazuri kwa nchi, wapo watu wamekuwa mabilionea kutokana na madini ya Tanzanite ambao hata sio watanzania lakini mzee amebaki hivyo hivyo
Rais amesema amepata taarifa hiyo kupitia meseji na baadae kupata taarifa kupitia mtoto wake Hassan Ngoma na alipochunguza wakakuta ni kweli
Rais anasema madini hayo yalikuwa yanasombwa na kama ni kuisha ungekuta yameisha
Sasa wataweka kamera na fensi ya umeme na ukuta huo utalindwa na JKT kwa kuwa ndio walioujenga na wanaujua vizuri
Rais anasema kuna makumpuni 1,700 yaiyosajiliwa ikiwepo Tanzanite One ila ni makampuni 25 tu ndio yalikuwa yakilipa, Tanzanite One pia wamekuwa wakiibia serikali
Anaishukuru kamati za madini za bunge kwa kufanya kazi nzuri na kusema wameijenga nchi kwa vitendo kwani tumechezewa mno
Rais anasema katika utafiti uliofanywa unaonyesha uchimbaji wa Tanznite utaendelea kwa miaka 27 ijayo,
Kuna eneo lingine ambalo hatalitaja ambalo lina Tanzanite nalo watalijengea pia ukuta, anasema watalinda kila penye mali na kama ikiwezekana hata Mlima Kilimanjaro pia wataujengea ukuta ili ifahamike kuwa upo Tanzania
Rais anasema pia Tanzanite imetoa ajira 30,000 huko India lakini hana uhakika kama wananchi wa Simanjiro wamefaidika na madini hayo kama walivyonufaika India
Stamico na Tanzanite one walitaka kuuza madini ila akawazuia mpaka sheria mpya ipitishwe
Kamishna wa madini alikuwa akiharakisha ila Rais akamharakisha yeye kwa kumuondoa akafanye kazi nyingine kwa kuwa kulikuwa na mchezo mchafu uliokuwa unafanywa
Rais amesema wataweka miundombinu itakayiwezesha wananchi wa Simanjiro kunufaika na biashara ya madini ya Tanzanite kwani wafanyabiashara wanaonunua madini hayo wamekuwa wakienda Arusha mjini au Dar
Rais Magufuli anazungumzia utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu bure na ujenzi wa miundombinu ya barabara na usambazaji wa umeme
Anasema kufikia mwaka wa 2020 hadi 2021 vijiji vyote vya Manyara vitakuwa na umeme, vijiji 273 vitapelekewa umeme
Rais anasema serikali imejipanga kwa ajiliya kuendeleza nchi hii, na awamu ya tano inapigana na vita ya uchumi ambayo inawagusa mabeberu mbalimbali na hawatafurahi
Rais anasema wengine ni mataifa ya kutoka nje na yataleta vitimbwi vya kila aina, wengine watakuja kwenye mambo ya vyama
Rais anasema wapo wanaotaka Tanzania isiendelee, wapo walioshangilia kukamatwa kwa ndege ya Tanzania na kuwaita ni mashetani
Rais anasema Watanzania waige vijana wa JKT walioonyesha uzalendo kwa kujenga ukuta na uzalendo ndio utakoilinda nchi
Rais anakabidhi gari la wagonjwa kwa mkurugenzi na kumuita mwenyekiti wa kijiji na kuwakabidhi gari la wagonjwa kwa pamoja
Mzee Jumanne Ngoma anatoa shukrani kwa rais kumtambua na kusema kuwa alikuwa chaguo la Mungu





Comments

Popular posts from this blog

Jacob Zuma resigns as South African President